28 Machi 2015 - 18:47
 Ndege ya Ujerumani iliangushwa kwa makusudi

Uchunguzi wa wataalamu wa Ufaransa unasema kile kinachodaiwa kuwa kitendo cha makusudi cha kuangusha ndege ya abiria ya shirika la ndege la Germanwings kilichofanywa na rubani mwenza katika maeneo ya milipa ya Alps ni "chanzo muhimu" kwa uchungizi lakini sio chanzo pekee.

Uchunguzi wa wataalamu wa  Ufaransa unasema kile kinachodaiwa kuwa kitendo cha makusudi cha kuangusha ndege ya abiria ya shirika la ndege la Germanwings kilichofanywa na rubani mwenza katika maeneo ya milipa ya Alps ni "chanzo muhimu" kwa uchungizi lakini sio chanzo pekee. Mkuu wa polisi Jean-Pierre Michel aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba wana miongozo kadhaa yenye kuwawezesha kuendelea na uchunguzi wao. Ndege hiyo ilianguka Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu wote 150 waliokuwemo katika ndege hiyo. Rubani wa ndege hiyo anatuhumiwa kumfungia mwenzie mlango kwa ndani kabla ya ajali ya ndege hiyo iliyosababisha hasara kubwa.